2 Samuel 22:1-6

Wimbo Wa Daudi Wa Sifa

(Zaburi 18)

1 aDaudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. 2 bAkasema: Bwana ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu,

3 cMungu wangu ni mwamba wangu,
ambaye kwake ninakimbilia,
ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.
Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu
na mwokozi wangu,
huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

4 dNinamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.


5 e“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

6 fKamba za kuzimu
Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho.
zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili.
Copyright information for SwhKC